dc.description.abstract |
Idadi ya ng'ombe Tanzania inakisiwa kufikia millioni 17.7 ambao wengi wao ni ngombe wa kienyeji aina ya "zebu". Idadi ya ng'ombe wa kisasa wa maziwa au machotara yao
na ng'ombe wa kienyeji ni kama nusu millioni tu. Ingawa ng' ombe wa kienyeji wana umbo dogo na hawatoi maziwa mengi kwa mkamuo ukilinganisha na wale wa kisasa,lakini wanastahimili zaidi hali ya joto na magonjwa katika nchi za tropiki kama Tanzania. Hata hivyo kuna matatizo kadhaa yanayofanya uzalishaji wa maziwa na nyama kwa ng'ombe wa kienyeji kuwa kidogo. Mengi ya matatizo hayo yanatokana na mbinu duni za ufugaji na hivyo kupelekea kuwepo kwa magonjwa mbalimbali na pia lishe duni kwa mifugo hasa wakati wa kiangazi. Kupungua kwa malisho bora wakati wa kiangazi kunajidhihirisha wazi katika sehemu nyingi za nchi yetu kwani mwaka baada ya mwaka
imekuwa kawaida kwa mifugo kunona na kutoa maziwa mengi wakati wa masika lakini mifugo hiyohiyo hukonda na kutoa maziwa kidogo sana wakati wa kiangazi. Ni dhahiri
kuwa kama wafugaji-wakulima wadogowadogo nchini wakizingatia kanuni za ufugaji bora, ikiwa ni pamoja na lishe bora kwa mifugo hasa wakati wa kiangazi, basi uzalishaji
wao utaongezeka kwa sababu ya idadi yao kuwa kubwa. |
en_GB |